ASSAs

RC MAKONDA AWATAKA WANAFUNZI KUACHANA NA MITANDAO YA KIJAMII

242
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wanafunzi kuachana na mitandao ya kijamii badala Yake kutilia mkazo katika masomo ili kuweza kulisaidia taifa siku za baadae.

Makonda amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam na Wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Msingi ya mzimuni alipokuwa katika ziara ya kukagua mirada yote iliyopo ndani ya Mkoa huo.

Amesema ili waweze kufanya vizuri katika masomo wanatakiwa kuweka juhudi, nidhamu pamoja na malengo binafsi, ambapo amewataka wanafunzi hao kufanya vizuri ili Rais Dkt.John Joseph Magufuli kuweza kujivunia wanafunzi waliopo katika chi yake.

“Mnauwezo mkubwa Sana wakufanya vizuri achaneni na tibia za kukaa kwenye mitandao ya kijamii wekeni bidii kwenye masomo ili mje kulisaidia Taifa, kuna mambo matatu ukiwa nayo lazima utafanya vizuri unatakiwa kuwa na Juhudi,Nidhamu pamoja na malengo, malengo yako lazima yawe tofauti na Dunia” amesema RC Makonda.

Aidha katika ziara hiyo pia alitembelea miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Soko la Magomeni,Ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Mzimuni, Ujenzi wa Zahanati Kigogo, Ujenzi wa Barabara na mitaro,Ujenzi wa Barabara kituo cha mabasi cha simu 2000.

Amesema ipo miradi inayofanya vizuri ikiwepo Soko la Sinza pamoja na Barabara ya simu 2000, ambapo amewataka watumiaji wa barabara hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho ujenzi unaendelea.

Pia amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kushughulikia changamoto za malipo kwa wa Vibarua rwanaofanya kazi katika miradi hiyo huku akiwaweka sawa mailpo halali wanayotakiwa kulipwa kuwa ni kiasi cha shilingi 12,500 na si chini na hapo.

“Tuna matumaini makubwa sana kutokana na kasi wanayoenda nayo na nampongeza sana DC kwa kazi anayoifanya, barabara ya kite cha simu 2000 pia inaendelea vizuri na kuna kipande cha mita 250 kimechukuliwa na TANROADS kwa jailli ya kuunganisha na ujenzi wa barabara ya Ubungo hivyo wanachi wakiona kinachelewa wasipate wajue mambo mazuri yanakuja”.

Ziara ya kukagua miradi ndani ya Mkoa huo bado zinaendelea ambapo siku ya kesho RC Makonda ataendelea na ziara katika wilaya ya Kinondoni.

(Visited 19 times, 1 visits today)
Share this post