ASSAs

RC MBEYA AMEWATAKA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUTILIA MKAZO SUALA LA UKUSANYAJI WA MAPATO

238
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert. Chalamila awewataka wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanajitathimini juu ya Malengo waliyojiwekea katika suala la ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri zao ikiwa ni pamoja na kupitia vyanzo vyote vya mapato kwa kutumia mashine za kierekroniki.

Chalamila ametoa kauli hiyo Leo wakati akifungua Mkutano kwa watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya unaolenga kujadili namna ya usimamizi wa shughuli za kifedha za Umma katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Rungwe.

“Anapokuja Mh Rais lazima wakurungenzi muwe na taarifa sahihi katika maaneo yenu ,hatutishani lakini uji amini na eneo lako sio unaulizwa Mkurugenzi hebu eleza mradi ule unasema hebu nimuite injinia pale pale utasikia injinia wewe ndio unakuwa Mkurugenzi nenda kwenye ofisi ya Mkurugenzi na wewe Mkurugenzi nenda kwenye ofisi ya injinia.”Amesema RC Chalamila.

“Mradi huu wa uboreshajj katika usimamizi wa shughuli za Fedha za Umma unamalengo ya kuboresha utendaji kazi katika Serikali za Mitaa kwa ujumla wake ili ziwe na uwezo mkubwa wa mapato yake ,lakini pia kuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza baadhi ya miradi yake kwa kutumia fedha za ndani.”

Muhimu zaidi amewataka wakurugenzi kuwa na taarifa sahihi katika maeneo yao pamoja na kutiia Mkazo juu ya usimamizi wa fedha na kujitathini katika malengo waliyojiwekea kuhusu ukusanyaji wa mapato.

(Visited 14 times, 1 visits today)
Share this post