ASSAs

RC MKOANI MBEYA ATOLEA UFAFANUZI KUTEKWA NA KISHA KUUWAWA KWA MTOTO JUNIOUR

1202
0
Share:

Ni kweli kuwa mnamo tarehe 9/4/2019 iliripotiwa taarifa ya kupotea kwa mtoto aliyejulikana kwa jina la Junior Siame ambapo kupotea kwake ilikuwa katika mazingira ya kutekwa na mtu asiyejulikana. Hivyo Jeshi la Polisi chini ya Uongozi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya -Kamanda Matei walianza kazi ya kupeleleza ili kujua mtekaji na hali ya mtoto Kwa siku hiyo.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na watu wa mitandao ya simu walifanya juhudi kubwa kubaini mtoto alipo.

Jinsi Ilivyokua:-

Tarehe hiyo alitokea mtu asiefahamika akamchukua mtoto aliyekuwa anakwenda Tuition. Baada ya kumchukua mtekaji alimpeleleza mtoto mambo mengi kuhusu hali ya maisha ya wazazi wake. Mtoto alimweleza mtekaji kwamba Baba yake ana gari ndipo wakatoka walipokuwepo wakaenda mpaka nyumbani kwa mtoto huyo ambapo mtoto aliingia ndani na mtekaji alibakia nje kwa kujificha. Mtekaji alifanikiwa kumrubuni mtoto aingie ndani kubadilisha nguo kisha atoke ili waondoke.

Junior aliingia ndani na kisha alibadili nguo na kutoka kisha waliondoka na mtekaji hadi maeneo ya nanenane.

Walipofika nanenane walipanda gari na kuelekea maeneo ya UYOLE mpaka mlima nyoka. Walipofika jirani na mlima nyoka mtekaji alianza kupiga simu Kwa wazazi kwamba mtoto anaye ili wampe milioni 10 ndipo amrudishe mtoto… Wakati akipiga siku mtoto JUNIOR alisikia na kugundua kuwa ametekwa na akaanza kulia.

Mtekaji baada ya kuona mtoto ameanza kulia akampeleka Porini kidogo ili kelele zake zisimuumbue. Baada ya hapo yule mtekaji alimbana mdomo iliyosababisha mtoto akazirai. Baada ya hapo yule Mtekaji alimvua mtoto track suit yake na kuanza kumpepea akijua amezimia. Alipoona mtoto amefariki aliondoka mpaka uyole na kupanda magari ya mizigo kuelekea Makambako- hadi Iringa. Akiwa huko Iringa aliendelea kupiga simu kwamba apelekewe hela kisha amrudishe mtoto.

Jeshi la Polisi lamnasa:-

Jeshi la Polisi ndipo likaongeza kasi ya kumsaka na ndipo jana tarehe 13/04/2019 likamtia nguvuni akiwa Iringa.

Historia ya Mtekaji:-

Mtekaji ni Mwenyeji wa Sumbawanga aliyehamia. Imebainika kwamba Kwa muda mrefu alikuwa gerezani mkoa Mwingine akitumikia Kifungo Baada ya kubaka. Kwahiyo ana uzoefu wa uhalifu wa ubakaji. Lakini mwezi wa Pili mwaka Huu aliachiwa huru.

Uamuzi wake wa kuteka:-

Baada ya kukamatwa na jeshi la Polisi anadai kwamba alikuwa hana mtaji wowote na ameamua kumteka mtoto ili apate hela za kujikimu toka kwa mzazi. Na uamuzi wa KUUWA umetokea baada ya mtoto kuzibwa mdomo.

Mtekaji akiwa Iringa katika Guest ambayo alilala pia inasemekana alijaribu kufanya ubakaji (bado vyombo vipo kazini kujua mtandao).

Usalama wa Jiji la Mbeya:-

Jiji la Mbeya ni salama sana na vyombo vya dola vipo kazini na ndiyo maana vimemkamata na ameelezaa kisa chote mpaka mauaji ya mtoto. Kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zingine za kisheria.

Ushauri wangu kama RC Wazazi wote tuendelee kuwa wamoja katika kuwalinda watoto wetu na kuwaonya wasiambatane na mtu wasiyemfahamu. Ni muhimu kuwafundisha kumkimbia kabisa mtu wasiyemjua. Na akina dada na hasa wale ambao wanaamini Maisha katika biashara ya Mapenzi wajue kuwa wanapaswa kuwa na tahadhari Kwa sababu watu wengine wananuka damu za watu kwahiyo hawezi kuogopa kumuuwa yoyote anaekuwa nae chumbani. Amani ya Mkoa wetu ipo mikononi mwetu wenyewe.

Hitimisho

Wana Mbeya wenzangu kitendo hiki kinatia huruma na kinachukizaa sana dhidi ya watu wa aina hii. Niwahakikishie kuwa vyombo vya Ulinzi na usalama vipo kazini wakati wote. Toa taarifa haraka unayooona kuna mazingira ya watu Kutishia amani iliyopo. Nawapa pole snaa snaa mzazi wa mtoto.

Nawapa pole sana Majirani, nawapa pole sana walimu na jamii yote. Serikali yetu imeumizwaa na itahakikisha Sheria kali zinachukuliwa kama malipo stahiki Kwa Mtekaji na muuwaji. MUHIMILI WA MAHAKAMA uendelee kutusaidia watu wenye makosa kama hayo hawastahili hata kidogo kutoka nje ya magereza mpaka kifo kitapowatenganisha na Magereza hizo.

Tukio hili halina uhusiano wowote na visasi vya kidini kama ilivyoripotiwaa. Bwana ametoa na shetani huyu ametwaa roho ya mtoto wetu Junior. R.I.P Pole sana BAKARI SIAME BABA WA MTOTO. TUENDELEE KUWA WAVUMILIVU WAKATI JESHI LA POLICE LIKIKAMILISHA SHUGHULI ZOTE ZA UPELELEZI NA HATUA ZINGINE ZA KISHERIA DHIDI YA MTUHUMIWA. TUENDELEE KUWA NA IMANI NA VYOMBO VYA DOLA HASA JESHI LA POLICE.

(Visited 151 times, 1 visits today)
Share this post