ASSAs

‘SISI WABUNGE HATUJAMUAGIZA SPIKA AENDE KUMUAMBIA CAG AKAJIELEZE KWA RAIS’ MBOWE

2678
0
Share:

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema yapo maamuzi magumu yanapswa kufanywa ndani ya taifa.

Mbowe ametoa kauli hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari, amesema kwa sasa Bunge linaendeshwa kama mali bifasi.

Amesema kwamba hata mambo yanayoendelea hivi sasa, Bunge halijamtuma Spika kufanya anayoyafanya, “pamoja na udhaifu wa bunge sisi wabunge hatujamuagiza Spika aende kumuambia CAG kwamba akajieleze kwa Rais, hayakuwa maazimio ya Bunge.

Mbowe amesema kwa sasa wapo kwenye kipindi cha bunge kinachojadili mambo ya msingi kwa mustakabali wa taifa na siyo kujadili maoni ya Watanzania.

Pamoja na hayo ameitaka serikali kuacha siasa za chafu kwa kuwafungia wapinzani huku chama tawala wao wakiendelea kufanya siasa za wazi.

(Visited 1,043 times, 1 visits today)
Share this post