ASSAs

RAIS WA UFARANSA AOMBA MSAADA WA KUJENGA UPYA KANISA LILILOTEKETEA NA MOTO

868
0
Share:

Rais wa Ufaransa ameahidi usaidizi wa kimataifa katika kulijenga upya kanisa kongwe la Notre Dame mjini Paris baada ya sehemu ya kanisa hilo kuteketea moto na kuharibika, moto ambao ulidhibitiwa saa tisa baada ya kuanza ambapo chanzo chake hakijajulikana.

Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema inachunguza mkasa huo kama ajli kwa sasa. Afisa mmoja wa zima moto alijeruhiwa kiasi wakati akikabiliana na moto huo, kamanda Jean-Claude Gallet ameiambia televisheni ya BFM.

Moto mkubwa ulizuka katika kanisa hilo kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa mwendo wa saa kumi na mbili na nusu kwa saa ya huko – jengo ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka ambapo  sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na moto huku mwingine ukifanikiwa kuzimwa katika minara miwili ya kengele.

Rais wa  Ufaransa Emmanuel Macron,ambaye alifika katika eneo la tukio amesema mawazo yake yako na “waumini wote wa kanisa katoliki na wafaransa wote kwa ujumla.”

“Sawa na watu wengine nchini , nimesikitika sana kuona sehemu ya maisha yetu ya kila siku ikiteketea.”

Bw. Macron awali alifutilia mbali hutuba mmuhimu kwa taifa kufuatia moto huo, alisema afisa wa Élysée Palace.

Msemaji wa kanisa hilo pia amekiri kuwa sehemu kubwa imeteketea na bado inaendelea “kuteketea”.

Mwanhistoria Camille Pascalameliambia shirika la habari lla Ufaransa BFMTV kwamba moto umeharibu ”turathi ya kitaifaKanisa hili limedumu Paris kwa takribani miaka 800, matukio ya furaha na ya kusikitisha kwa karne kadhaa yamekua yakiadhimishwa kupitia mlio wa kengele za Notre Dame, tunasikitishwa na kile kilichotokea na kile tunachojionea”.

Maafisa wa zima moto walifanikiwa kuliokoa jengo hilo la historia lenye miaka 850 lakini paa na mnara wa jengo hilo yameanguka.

(Visited 65 times, 1 visits today)
Share this post