ASSAs

RC MAKONDA AAGIZA MADIWANI WA ILALA KUSIMAMIA MIRADI YA MKAKATI

759
0
Share:

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Poul Makonda amewagiza Madiwani wa Halmashauri ya Ilala kusimamia miradi ya mikakati ya Serikali ili iweze kukamilika kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa mapema jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha zarura cha Baraza la madiwani Ilala kilichoitishwa ili kujua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na manispaa hiyo.

“Nawapongeza Manispaa Ilala kwa kuanza ujenzi wa miradi mkakati ya serikali ni hatua nzuri hivyo ongezeni bidii muweke nguvu kwa pamoja “amesema Makonda.

Aidha amesema, wamempata Rais ambae anapenda Maendeleo ambapo miradi ya maendeleo imeibuliwa katika ILANI ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa hivyo itekelezwe kwa wakati.

“Nimepata ajira ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli hivyo tuweke nguvu ya pamoja ili tusimwangushe Rais wetu wa awamu ya tano katika kasi ya maendeleo “amesema Makonda.

Hata hivyo, amewataka madiwani wa Ilala wawe kitu kimoja wasonge mbele wasikwame kokote katika kusimamia miradi, huku akimtaka Mkurugenzi wa Ilala
kuondoa wakandarasi ambao wanalalamikiwa, badala yake wachukue mkandarasi mwengine ili shughuli za ujenzi zisikwame kwa kisingizio chochote.

Katika hatua nyingine, amemwagiza Katibu TAWALA Mkoa wa Dar es Salaam hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu kuwahamisha wakuu wa idara walioshindwa kazi katika Mkoa huo.

Kwa upande wake, Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, wakati akisoma Taarifa za Manispaa ya Ilala amesema hadi Februari mwaka huu pesa iliyotoka ya mikopo shilingi milioni 153 kwa vikundi 44 ambapo changamoto kubwa vikundi vingi vilikuwa havina vigezo mpaka kufikia sasa shilingi bilioni 1.7 zimeandaliwa kwa vikundi 295 kati ya vikundi hivyo vya wajane 28.

Kumbilamoto amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 700 zimeingizwa na zinaendelea kuingizwa katika akaunti za vikundi ambayo vimehakikiwa akaunti zao.

Amesema kuwa, mpaka kufikia Mei 30 mwaka huu vikundi 500 vitakuwa tayari vimepewa mkopo ya Serikali ndani ya Manispaa ya Ilala zaidi ya bilioni 4.1zimetengwa kwa ajili ya mikopo hiyo, Aprili 17 Mkuu wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA anatarajia kutoa mikopo awamu ya pili ikiwemo Bajaji, Bodoboda kwa vikundi vilivyomba mikopo zaidi ya 200 Katika viwanja vya Mnazi mmoja.

(Visited 49 times, 1 visits today)
Share this post