ASSAs

ILALA YATOA MKOPO WA SHILL BILL 1.7, YAVITAKA VIKUNDI KUREJESHA FEDHA KWA WAKATI

339
0
Share:

Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amevitaka vikundi vilivyopata mkopo wa uwezeshaji kiuchumi uliotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kutumia mkopo huo kwa malengo yaliokusudiwa ili waweze kurudisha fedha hizo kwa wakati na wengine waweze kupata.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam, wakati alipokua akitoa mikopo wa vitendea kazi wenye thamani ya shilingi billioni 1.7 kwa vikundi mbalimbali vikiwemo vya wanawake, vijana, walemavu, wajane pamoja na wasanii waliopo katika Manispaa ya Ilala,

Amesema kuwa, endapo mikopo hiyo wataitumia kwa malengo yaliokusudiwa basi ndani ya muda mfupi wataweza kurejesha fedha kwa wakati na manispaa itaweza kuwapa mkopo mkubwa zaidi.

“Leo tumetoa mkopo wa shilingi bilioni 1.7 lakini lengo letu hadi kufikia mwezi wa Mei tunataka tuwe tumetoa mkopo wa shilingi bilioni 4, hii ni ishara wale watakao rudisha fedha kwa wakati wataweza kupata mkopo mkubwa zaidi”amesema Mjema.

Ameongeza kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha wanawawezesha kiuchumi watanzania ili wawe na maisha mazuri jambo ambalo litaleta tija kubwa sana kwani wataweza kujiajiri wenyewe kupitia mkopo huo ambao unatolewa bila riba kwa Tanzania nzima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri amevitaka kikundi hivyo kuhakikisha wanarejesha fedha kwa wakati ili na wengine waweze kupata,ambapo amesema bajaji na pikipiki walizotoa wamezikatia bima kubwa.

Aidha amesema kuwa, vikundi vyote wamewapatia elimu ya kurejesha mikopo hiyo kwa wakati, ambapo amebainisha endapo watazitunza vizuri wataweza hata kununua zakwao wenyewe baada ya miaka 5

Naye Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amesema zoezi lilifanyika leo ni kutimiza ndoto ya Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha kila mtanzania anakua na maisha mazuri, hivyo amevitaka vikundi hivyo kumpongeza kutokana na kasi ya ajabu anayokwenda nayo kwani ameahidi na ametekeleza kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa vitendo.

Amesema kuwa, leo wametoa mikopo yenye thamani ya Shilingi billioni 1.7, ambapo awali walitoa mkopo wa shilingi milioni 153 kwa vikundi mbalimbali, huku lengo likiwa ni kufikia kutoa mkopo wa shilling 4.1 hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu.

“Katika mkopo huu wa leo wa uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, pia hatujawasahau wasanii na wajane ambao wapo 208 na wamejiunda katika vikundi vyao na vipo 28 wataweza kupata mikopo hii muhimu ni kurejesha fedha kwa wakati na wengine wapate ” amesema Kumbilamoto

Ameongeza kuwa, mikopo hiyo ya bajaji wameamua kuiweka nembo ya Manispaa ya ilala, ili kuwaonesha wananchi nini wanafanya kumsaidia Rais John Magufuli kwani hata wafanye mazuri mangapi hayaonekani wala hayasemwi lakini wanapokosea kidogo tu wanaanza kutangazwa kwenye mitandao.

(Visited 36 times, 1 visits today)
Share this post