JUSTIN BIEBER MAHAKAMANI KWA KUMGONGA NA GARI MPIGAPICHA

Mwanamuziki maarufu wa Canada, Justin Bieber, ameshitakiwa kwa kumngonga na gari mpigapicha mmoja wakati akitoka kanisani mjini Los Angeles, Marekani, mwaka 2017. ambapo mtandao wa The Blast umeripoti.
Kutokana na taarifa za mpiga picha huyo anayefahamika kwa jina la William Wilson ni kwamba alikuwa amesimama upande wa waenda kwa miguu kabla ya ajali hiyo ambayo imemsababishia ulemavu na matatizo ya kisaikolojia
Waandishi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walimuhoji Msanii huyo na akaweza kujitetea kwa kuwaambia kuwa hakufanya hivyo kwa makusudi bali ni kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa nayo siku hiyo.
(Visited 70 times, 1 visits today)