ASSAs

KANGI LUGOLA AWATOA HOFU WAJAWAZITO WALIOPO GEREZANI

253
0
Share:

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola amewawatoa  watu hofu juu yafungwa waliokuwepo gerezani ambao ni wajawazito na  kupelekea wengine kujifungua wakiwa gerezani.

 Baada ya Mbunge kuhoji juu ya huduma za  wafungwa wajawazito waliokuwepo gerezani Lugola amesema jeshi la magereza limekuwa likitoa huduma kwa wafungwa embat ni wajamzito hasa chanjo na kumruhusu kuhudhuria kliniki za mama wajawazito ili kuhakikisha Afya inaimarika

“Jeshi la magereza limekuwa likihifadhi wafungwa wa aina zote wakiwemo wafungwa wa kike wajawazito katika kuhakikisha kwamba wafungwa wajawazito wanajifungua salama, jeshi la magereza limekuwa likitoa huduma za Afya chanjo na kuhakikisha wanahudhuria kliniki za mama wajawazito katika vituo vya Afya vya magereza na pale inapobidi kuwapeleka Hospitaku za Serikali”

Aidha amesema Kuwa bali na kuwasihi mama wajawazito kuhudhuria kliniki wamekuwa wakiwapatia vyakula wanavyohitaji kwa kuzingatia ushauri wa daktari wa magereza ili kuilinda Afya ya mama na mototo

“Jeshi la Magereza limekuwa likiwapatia wafungwa wajawazito vyakula wanavyovihitaji kiafya kwa kuzingatia maelekezo na ushauri wa daktari wa gereza kuhakikisha Afya ya mama na mtoto inalindwa

Kagi Lugola amemaliza kwa kusema kwamba  wakinamama wafungwa ambao wanajifungua watoto wakiwa gerezani utaratibu wa jeshi la magereza kupitia kanuni za jeshi la magereza wanao utaratibu  kwa watoto ambao wamekwishazaliwa gerezani, wanapofikia umri wa kuanza shule ya awali wanakuwa wakisoma shule za awali zilizoko kwenye magereza  na kupewa ushauri ili wasijihisi nao ni wafungwa kwakuwa wamezaliwa gerezani.

(Visited 14 times, 1 visits today)
Share this post