ASSAs

MANISPAA YA TEMEKE WAPONGEZA JITAHIDI ZA RC MAKONDA

245
0
Share:

Mstahiki Meya Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo amesema mafanikio wanayopata ndani ya wilaya hiyo ni kutokana na juhudi  na umakini uliopo kwa madiwani, wenyekiti pamoja na ushirikiano mzuri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Chaurembo amezungumza hayo mapema leo mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Kukagua miradi ya Maendeleo iliyopo ndani  ya Mkoa wa Dar es Salaam, inayokaguliwa na Rc Makonda, amesema anaamini eneo lolote lenye ushirikiano mzuri lazima kutakuwa na Maendeleo mazuri.

“Tunaamini mafanikio yet tuliyonayo katika miradi iliyopo ndani ya wilaya yetu ni kutokana na umakini mkubwa na usimamizi mzuri tulionano kwa kushirikiana na madiwani,wenye viti lakini nchini ya Usimamizi wa Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, nitoe wito kwa halmashauri nyingine waje Temeke wajifunze baadhi ya vitu kutoka kwetu” amesema Chaurembo.

Katika hatua nyingine diwani  kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika Jimbo la Chang’ombe Benjamini Ndalichako ametangaza kujivua uanachama pamoja na kujivua udiwani ikiwa sambamba na nafasi zote alizokuwa nazo ndani ya chama hicho na kutangaza kuhamia chama cha Mapinduzi CCM.

Amesema kuwa ameamua kuondoka chama hicho akiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali zinazofanywa chini ya Rais Dkt John Magufuli, ambapo ameeleza kuwa ameamua kufata maendeleo na kuachana na siasa.

“Leo tulikuwa na ziara ya kukagua mirada ya maendeleo na Mkuu wetu wa Mkoa, tunagombea vyeo vya siasa ili tulete maendeleo unapoona nguvu inaongezwa zaidi kutokana na maendeleo haya mimi nimejivua nafasi yangu ya udiwani na nafasi zote nilizokuwa nazishikilia na kumuunga mkono Rais kwa kazi nzuri anayoifanya kwa miradi mbali mbali” amesema Ndalichako.

(Visited 19 times, 1 visits today)
Share this post