ASSAs

RC MAKONDA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BWENI NA MADARASA SHULE YA WATOTO WENYE ULEMAVU WA MACHO

264
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Madarasa,Mabweni,pamoja na Vyoo mahususi kwa watoto wenye ulemavu wa Macho pekee katika shule ya msingi Toangoma iliyopo katika halmashauri ya Temeke ikiwa ni Shule ya kwanza katika Mkoa huo.

Amesema shule hiyo itatoa nafasi ndani ya Mkoa pamoja na nje ya mkoa ambapo  ametoa wito kwa wazazi kutowaficha ndani watoto badala yake wawapeleke shule ili kuweza kupata elimu maana ni haki yao.

“Hongereni sana kwa kazi nzuri hiki mlichokifanya mtawasaidia wana Temeke mtawasaidia wana Dar es Salaam lakini pia mtalisaidia Taifa kwa Jumla, tuna fahamu changamoto kubwa sana kwa walemavu ni Elimu mlichokifanya sio tu Maendeleo lakini pia mmetekeleza hata maandiko matakatifu,.

Endapo Jango hili litakamilika basi basi hii odio itakuwa Shule ya pekoe kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika kutoka Elimu kwa walemavu wa macho” amesema.

Amezungumza hayo alipokuwa katika mwendelezo wa ziara  ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo ametembelea baadhi ya miradi katika halmashauri ya wilaya ya Temeke, Ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara, ujenzi wa vyoo, madarasa pamoja na mabweni katika shule ya msingi Toangoma itakayokuwa maalumu kwa watoto wenye ulemavu wa macho.

Pia ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kisima unaotarajiwa kukamilika mei mwaka huu kilichoko katika Kata ya Charambe, pamoja na kituo cha Afya cha Ghorofa 3 kilichopo katika kata ya Yombo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu matumizi ya fedha katika ujenzi wa shule ili kuhakikisha inakamilika kwa muda muafaka, amesema Mpaka saa ujenzi wa Bweni hilo na madarasa yamefikia 97%  ili kuweza kukamilisha ujenzi huo, ambapo amesema Bweni hilo litabeba Jumla ya watoto 80 na kusema kwasasa katika shule hiyo ina watoto 24.

Amesema lengo si kuangalia wenye ulemavu wa macho tu bali ni kugusa watoto wote wenye ulemavu wa viungo na kuhakikisha wanapata elimu, pia ametoa shukurani kwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kusimama na kuwasaidia kila wanapohitaji msaada wa Maendeleo katika halmashauri hiyo.

“kwasasa tumeanza na jengo litakalo hifadhi jumla ya watoto 80, tuna mpango Mungu akipenda tutaendelea zaidi lento letu ni kuhakikisha tunatoa nafasi kwa watoto wote wenye matatizo ya viungo mimi kama Mkurugenzi naahidi nitapambana hadi senti ya mwisho nikishirikianana Rais wangu Dkt. John  Magufuli” Amesema Mwakabibi.

Ujenzi wa shule hiyo ya walemavu unatarajiwa kugharamia kiasi cha shilingi milioni 120 kwa majengo matano na kwamba mpango mkakati uliopo ni kuhakikisha wilaya ya Temeke inajenga takribani shule tano za watu wenye ulemavu.

 

(Visited 23 times, 1 visits today)
Share this post