ASSAs

SAHARA TANZANIA LIMITED YAANZISHA KAMPENI KUWASAIDIA SERENGETI BOYS

1655
0
Share:
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Sahara Wakiongozwa Afisa Maendeleo ya Biashara Bi Mwajabu Mrutu (Watatu Kulia) Wakiwa Kwenye Kampeni ya Kuwasaidia Vijana wa Serengeti Boys ili kuweza kufanya Vizuri Kwenye Michuano ya Kombe la Afrika (AFCON -U17) Inayoendelea Nchini.
 
KAMPUNI  ya Sahara Tanzania Limited imeamua kuanzisha kampeni ya kuwasaidia vijana wa Serengeti Boys kwa lengo la kuhakikisha wanafanya vema katika michuano ya Kombo la Africa (AFCON) chini ya miaka 17 inayoendelea nchini. Akizungmza leo Aprili 17, 2019 jijini Dar es Salaam Ofisa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo Mwajabu Mrutu amesema kampeni hiyo inajulikana kama ‘KeepYourEyeOnTheBall’ ambayo inatoa hamasa kwa vijana hao ili wajiamini na kufanya vizuri.Hivyo amesema kupitia kampeni hiyo,  Sahara Tanzania Limited inatoa msaada wa kuwajengea uwezo vijana hao wa Serengeti wanaoshiriki AFCON 2019.
 
“Licha ya kuwa tunatoa hamasa kwa vijana katika kufanya vizuri siku za usoni, pia tunatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kufanya vizuri zaidi,”amesema na kuongeza kampuni yao inatoa hudumu ya kuwapeleka wachezaji na mashambiki uwanjani kwa ajili ya kuwapa hamasa vijana wa Serengeti.Mrutu ametoa ombi kwa vyombo vya habari nchini na wadau  wengine wakiwemo mashabiki wa Serengeti Boys kusaidia katika kutekeleza kampeni hiyo inayolenga kuwasaidia vijana.KeepYourEyeOnTheBall’ si ujumbe wa wachezaji tu, tunaamini ni ujumbe ambao unakuja wakati mwafaka kwa vijana wote wa Tanzania kwa ajili ya kupenda na kuhamasika katika suala la  mpira wa miguu nchini Tanzania,”ameongeza Mrutu.
 
Wakati huo huo amesema kupitia kampeni hiyo, Sahara Tanzania Limited inatoa pia msaada wa masuala ya ujasiriamali na uchumi kwa ajili ya kuandaa wachezaji vijana kuona kama mpira ni sehemu nzuri ya kutengeneza maisha ya yao ya baadae.Tuna imani kuhusu vijana wa Tanzania na hii inatufanya  Sahara tuendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia maendeleo endelevu kwa vijana  wetu,” amesema.Amefafanua kuwa Sahara Tanzania Limited kupitia Sahara Foundation inatekeleza miradi mbalimbali nchini ukiwemo mradi wa kupandisha  hadhi maabara katika Shule ya Sekondari Pugu inayohudumia wanafunzi  zaidi ya 1000. Miradi mingine ni School Sanitation Wash and Hygiene (SWAH) ambao unahusisha utoaji wa vyoo na bafu katika shule ya Sekondari ya Salma Kikwete.
(Visited 198 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us