ASSAs

WATU 150 HAWAJULIKANI WALIPO BAADA YA BOTI KUZAMA MAJINI

267
0
Share:

Rais wa DR Congo amesema takriban watu 150 wametoweka huku wengine 33 kuokelewa  baada ya boti waliokuwa wakiabiri kuzama katika ziwa moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Rais huyo amesema Kuwa amehuzunishwa sana na kuzama kwa boit hilo kwani imesababisha kupoteza maisha ya watu ambao hadi sasa hawajajulikana wapo patika hali gani.

”Nimehuzunishwa na kuzama kwa boti hiyo tarehe 15 mwezi Aprili katika ziwa Kivu. Hadi kufikia sasa idadi ya watu ambao hawajulikani waliko ni 150” , alisema rais wa taifa hilo Felix Tshisekedi katika akaunti yake ya Twitter.

Kulingana na mwanaharakati mmoja katika eneo la Kivu kusini ambaye alikuwa akizungumza na shirika la habari la Reuters, boti hilo ambalo lilikuwa limetoka katika mkoa jirani wa Kivu kaskazini lilizama katika ziwa hilo karibu na eneo la Kalehe.

Tshisekedi amesema kuwa anaifuatilia kwa karibu hali hiyo ili kuwatambua na kuwachukulia hatua wale waliohusika.

Mikasa mibaya ya ajali ya maboti ni swala la kawaida nchini DR Congo na Reuters mwaka uliopita , boti moja lilipinduka katika mto kaskazini mwa DR Congo , na kusababisha watu 49 kufa maji huku idadi kama hiyo ya watu wakiokolewa.

(Visited 16 times, 1 visits today)
Share this post