ASSAs

HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA DIAMOND KWA BABA YAKE MZAZI

1771
0
Share:

Hatimaye msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amepatana na baba yake mzazi mzee Abdul Juma ambapo jana mzee huyo aliibuka kwenye studio za Wasafi FM na kukutana na mwanaye ambapo tukio hilo limetokea jana usiku wakati Diamond akifanya mahojiano na kituo chake cha Radio cha Wasafi FM kuhusu maisha yake na vitu vingine anavyofanya kuhusu kazi zake za muziki.

Akizungumzia tukio hilo, mzee Abdul amesema anajisikia faraja sana kupokelewa na mwanaye kipenzi hivyo faraja na furaha yake imerejea kuona mahusiano yao yamekuwa mazuri sasa huku akidai hali iliyokuwepo mwanzo ya kutoelewana ilikuwa ikimpa wakati mgumu na kusema kuwa anataka mambo hayo yaishe.

“Mimi ni mtu mzima huyu ni mwanangu siwezi kumuomba msamaha, nataka tu haya yaishe,” amesema mzee Abdul.

Baadhi ya mashabiki wamempongeza Diamond kwa uamuzi aliouchukua na kuendelea kumshauri aendelee kuelewana na mzazi wake siku zote.

(Visited 774 times, 1 visits today)
Share this post