ASSAs

ZARI AMJIA JUU DIAMOND, ATOA SIRI ZOTE

5414
0
Share:

 Zari Boss Lady,  amefunguka baada ya msanii Diamond kuongea mengi kuhusu mahusiano yao yaliyopita ndani ya kituo chake cha redio cha Wasafi FM jana,  April 23, 2019 ambapo  Diamond alifunguka mambo mengi ikiwemo Zari kum-cheat kwenye mahusiano, kuhusiana na kutoa sapoti kwa wanaye, na mambo mengine yaliyokuwa yanawahusu walipokuwa kwenye mahusiano.

Zari alituma video tatu kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa anamjibu mzazi mwenzie ambaye aliongea mengi kuhusu familia  na maisha yao kwa ujumla ambapo baadhi ya maneno yalissomeka hivi:

“Sasa yale magoti mpaka Sauzi yalikuwa ya nini? Kule  kuomba msamaha kwote kwa radio kwa nini? Kwani umekuwa comedian sasa? Usinichafulie maisha bro. Yameisha zamani kubali tu. Kiki zimekuwa ngumu mjini. Niheshimu tafadhali nakulelea watoto tena vizuri”.

Zari ameogelea kuhusu malezi na mawasiliano ya diamond  kwa watoto wake ambapo amesema kuwa Diamond amepewa namba zote za watoto wakubwa wa zari ili apate mawasiliano na watoto wake pale atakapohitaji kuwasiliana nao, Pia Zari amesema kuwa hajaelewa inakuwaje Diamond anapata moyo wa kujiamini kwenda kwenye media na kumdhihaki kwa kumsingizia kuhusiana na mahusiano ambayo hajashiriki.

Katika mahojiano aliyoyafanya Diamond alisema kuwa Zari alishawahi kuwa na mahusiano na msanii wa muziki Mr P wa Psqure ambapo zari amemjia juu na kumjibu kuwa  aendelee kukaa anapokaa kwakuwa anaishi maisha yake na anawalea vizuri watoto wake vizuri na  kuhusu mahisiano yake na  Mr P si ya kweli.

“Kama nyie watu mtaamini maneno yanayotoka mdomoni mwa mwanaume kama huyu, yule yule aliyekataa damu yake, anakimbilia kwenye radio, anafanya ziara, kama kweli mnamuamini mtu huyu basi nyie wote ni wapumbavu kama yeye.  Naomba tuheshimiane, kaa mahali ulipo, mi nipo nilipo, Mimi na watoto tupo vizuri bila wewe. Naomba tuheshimiane”.

(Visited 3,179 times, 1 visits today)
Share this post