ASSAs

MIMBA YA TANASHA YATIKISA MTANDAONI

2591
0
Share:

Mtangazaji kutokea nchini Kenya ambaye pia ni mpenzi wa sasa wa mwanamuziki Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ameibua gumzo katika mitandao ya kijamii kufatia muonekano wake kuonekana kama ni mjamzito.

Hivi karibuni mrembo huyo alitupia picha mtandaoni ambayo iliwafanya wadau wengi wa instargram kuikagua na kutoa majibu ya macho kuwa tayari ni mama kijacho.

Aidha, picha hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya waliokomenti waliishia kumpongeza kwa kukubali kuzaa na Mondi huku wengine wakimtahadharisha kuwa, asipoangalia yatamkuta yaliyowakuta waliomtangulia (Zari na Mobeto).

“Anabeba mimba kabla ya ndoa, asubirie kutoswa tu,” alikomenti mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Double J kwenye mtandao wa Instagram.  Mwingine akaandika: “Waoo shemeji langu la nguvu, zaa mama… zaa umzalie Simba, pesa ya kukutunzia ipo.”

Huko huko Insta baada ya Diamond kuona watu wakimpongeza mpenzi wake, naye alikomenti kwenye picha hiyo akisema: “Kileee, nakiona kwa mbali (akimaanisha anakiona kibendi kwa mbali).

(Visited 947 times, 3 visits today)
Share this post