ASSAs

CCM WAWEKA WAZI SIRI YA LOWASSA KUREJEA CCM

791
0
Share:

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amesema wakati Edward Lowassa alipotaka kurudi chama hicho, walimtaka kiongozi huyo kwenda kuomba ridhaa kwenye ngazi ya tawi, na wakimridhia ndipo aweze kurejea.

Dkt. Bashiru Ally ametoa kauli hiyo leo, jijini Dar es salaam, wakati akizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo suala la miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumzia suala la Lowassa kurejea CCM Dkt. Bashiru amesema kuwa “kuhusu waliorudi CCM, sharti la kwanza ukubaliwe uanachama kwenye tawi, suala la kukubalika kwenye tawi ni sifa mojawapo”

“Lowassa kurudi CCM kulikuwa na mazungumzo ndani ya chama baada ya kupokea maombi yake na wala hakuwa yeye peke yake” ameongeza Dkt Bashiru.

Machi 1, 2019 katika Makao Makuu madogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam, Edward Lowassa alitangaza uamuzi wa kurejea CCM baada ya kuondoka wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015.

(Visited 90 times, 1 visits today)
Share this post