ASSAs

WAZIRI MKUU ATANGAZA KUTOKUWEPO NA SHEREHE ZA MUUNGANO

333
0
Share:

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ametangaza kutokuwepo kwa shamrashamra za sherehe kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano leo April 26, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu imeweka wazi kuwa siku ya leo itatumiwa kama siku ya mapumziko ya kitaifa lakini hakutakuwa na sherehe zozote za kitaifa.

Aidha Majaliwa ameongeza kuwa fedha kiasi cha sh. milioni 988.9 zilizokuwa zitumike kwenye sherehe hizo, zimeokolewa na zitapangiwa matumizi mengine.

Tanzania kesho inaadhimisha miaka 55 tangu nchi za Zanzibar Visiwani na Tanganyika ziungane mwaka 1964, chini ya viongozi wa wakati huo Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume.

(Visited 33 times, 1 visits today)
Share this post