ASSAs

MKUU WA WILAYA YA ULANGA MHE NGOLLO MALENYA AKABIDHI VIFAA KWA WATAHINIWA WA KIDATO CHA SITA

529
0
Share:

Katika Jitihada za kuinua kiwango cha Elimu na Ufaulu Wilayani Ulanga Jana tarehe 26.4.2019 DC Ngollo Malenya alikabidhi vifaa vyenye thamani ya Tsh.3,765,000Mill Kwa Watahiniwa wa Kidato cha Sita Kwa Shule zilizopo Wilaya ya Ulanga ambao wanatarijiwa Kuanza Mtihani Wa Taifa hivi karibuni.Miongoni Mwa Vifaa ambavyo Mhe Ngollo aligawa vilikua ni Kalamu za Wino, Kalamu za Mkaa, Mosquito repellant, Sabuni za Kuogea na Kufulia Pamoja na Mahitaji Muhimu ya Watoto wa Kike kama nguo za ndani na taulo za kike.

Alisema lengo la Kugawa vifaa hivyo ni kuwapatia wakati mzuri wa maandalizi Watahaniwa na ili ufaulu uweze kuongezeka katika Wilaya ya Ulanga lakini pia alisema itawapatia Utulivu na kuwaondoa katika hali ya Usumbufu wa Mawazo juu ya Upatikanaji wa vifaa.

Pia DC Ngollo alimshukuru Mhe Raisi Magufuli Kwa Kuipa Elimu kipaumbele Kwa Kufanya jitihada mbalimbali za kuinua Elimu ”Maana hata vitabu vitakatifu vimetuasa Mshike Elimu asiende zake nasi Wana Ulanga tuthamini Elimu” alisema DC Ngollo.

Mwisho aliishukuru Kampuni ya Tanzigraphite Kwa Kuunga Mkono jitihada za Kuinua Kwa kujitolea vifaa hivyo na Kua ni Miungoni Mwa wadau Wakubwa wa Maendeleo ya Elimu katika Wilaya ya Ulanga.

(Visited 53 times, 1 visits today)
Share this post