ASSAs

MJADALA WA DAWA ZA KUONGEZA MAKALIO WAZIDI KUPAMBA MOTO BUNGENI

1055
0
Share:

Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amemzuia Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi kujibu swali la mbunge juu ya madhara wanayopata wanaume endapo wakikutana kimapenzi na wanawake waliotumia dawa za kuongeza makalio.

Hayo yametokea leo katika kipindi cha maswali na majibu, ambapo Waziri Mwinyi alikuwa akijibu maswali hayo kwa niaba ya Waziri wa Afya. Swali hilo lililozuiliwa majibu, Mbunge huyo alitaka kujua ni madhara gani ambayo ataweza kupata mwanaume pindi atakapokutana na mwanamke ambaye ametumia dawa za  kukuza makalio.

Hata hivyo kabla ya Waziri kutoa majibu ndipo Mwenyekiti Chenge akasema, “hilo swali hawezi akalijua yeye madhara hayo..Mmmnh…Waheshimiwa tunaendeleaa..”.

Pamoja na hayo Mbunge Suzan Lyimo naye alitaka kujua madhara yanayowakuta wanaume ambao wanatumia dawa za kukuza maumbile yao.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwinyi amesema kwamba, “taarifa zimekuwa nyingi za dawa za kukuza maumbile, watu waache kutumia dawa ambazo hazijathibitishwa kitaalamu kwani zitasababisha madhara. Kwa taarifa zilizopo hakuna dawa yoyote ambayo kitaalamu imepewa kibali kwa ajili ya matumizi kama hayo”.

Ameongeza, “Watanzania wameaswa kuacha kutumia dawa kama hizo kwani zinaweza kuwa na madhara. Nitoe wito pia kama kuna mtumiaji yoyote aliyewahi kupata madhara baada ya matumizi ya dawa hizo atoe taarifa”.

(Visited 91 times, 1 visits today)
Share this post