ASSAs

RAIS MAGUFULI AWEKA WAZI KITU KINACHOMNYIMA RAHA

1464
0
Share:

RAIS  John Magufuli ameeleza mambo yanayomuumiza juu ya timu za soka za taifa ambazo ni timu ya Taifa Stars na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys,  kufungwa na timu za mataifa mengine katika michuano mbalimbali ambayo imechezwa hivi karibuni na kusema kuwa anatamani siku oja angekuwa Waziri wa Michezo na kuweza kuipanga lizuri Timu

Magufuli amesema hayo leo Aprili 30, 2019 wakati wakiwahutubia wananchi wa Kyela mkoani Mbeya na kusema  kitendo cha kufungwa kwa timu hizo kimekuwa kikimnyima raha huku akimtaka waziri wa michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kufuta aibu hiyo ya kufungwa kila mara.

“Kukatika kwa umeme kunaumiza sana, unakuta unaangalia mpira umeme unakatika halafu goli linaingia, na Waziri wa Michezo anatoka huku Mbeya, ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha sana. Katika vitu ambavyo huwa vinaniudhi ni kufungwa timu zangu, huwa inaniuma mno, yani watu milioni 55, mnafungwa na timu ya nchi yenye watu milioni 33, hii ni aibu kubwa mno.

“Natamani siku moja niwe waziri wa michezo halafu niwaonyeshe mimi ni nani, kwanza kikosi nitakipanga mimi mwenyewe halafu tuone kama tutafungwafungwa tena, timu ya wakubwa nayo hivi karibuni itaanza mashindano, sijui nayo mechi ya kwanza tu itafungwa! Labda kufungwa nao ndiyo mchezo mzuri,” amesema Magufuli.

(Visited 186 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us