ASSAs

KOCHA MKUU WA TAIFA STARS AFANYA MAAMUZI KWA KELVIN MBAPPE

1363
0
Share:

. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amemuita Mbappe kwenye kikosi cha wachezaji 39 wanaounda kikosi kinachojiandaa na mashindano ya Afcon, pamoja na Chan.

Akilizungumza hilo Mbappe alisema kuwa alikutana na wakati mgumu baada ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kwa kuwa watu wengi walikuwa wanampigia simu huku WhatsApp yake ikipokea meseji zaidi ya 200 kwa muda mfupi.

“Sikulala kabisa, simu zilikuwa nyingi sana, inatoka hii inaingia hii, WhatsApp yangu ilipokea meseji zaidi ya 200 kwa wakati mmoja, mwisho wa siku nikaamua kuizima simu kabisa ili nipate nafasi ya kulala,” alisema Mbappe.

(Visited 610 times, 1 visits today)
Share this post