ASSAs

AFCON ISIWE KICHAKA TWENDENI KAZINI

413
0
Share:

Na Mohamed Ngangambe

Mtoto wa Nyoka ni Nyoka na asie na Mwana aeleke Jiwe ndio unapata picha gani hapa ukileta misemo hii katika hoja ya michezo ,unaweza kusema Brazili ni nyoka Na ndio maana kila siku wanafuzu Worldcup na wanafanya vizuri katika anga la michezo ,Angalia kizazi cha kina Pele mpaka sasa huyu Nyota Neymar yeye na wenzake wanatembelea tu nyota na mizizi Ya babu zao

Na Vipi Afrika Yetu hapa? Hapa nitakutajia Cameroon, Ghana ,Nigeria na Senegal, Mimi naanza na hawa, Steven Appiah wa Ghana, Sunday Oliseh, Patrick Mboma, Sibosiso Zuma, Mohamed Aboutrika, Wael Gomaa, Amr Zaki, Khalilu Fadiga wa Senegal

Na Tizama akina Didier Drogba, Samuel Etoo na hata Asamoh Gyan sawa wenzetu ni Nyoka .

Labda turudi hapa nyumbani msemo wangu wa pili ni asie na mwana aeleke jiwe kwa miaka mingi sana tumeeleka jiwe migongoni mwetu kwenye michezo tumekua namba moja kufuatilia na kuanikiza michezo na wanamichezo wa nje bila kuangalia nyumbani kwetu nasemaje! ule msemo wa Tanzania kichwa cha mwenda wazimu umetupa laana kubwa eeh! sana labdaaa! ndio wanasema mjomba amesema akisema amesema mama !mmh! sasa sijui yasingesemwa ila wakati mwingine tuache usemwe umetujenga mno !

Nije kwenye Jiko niandae chakula na tuanze kula msosi wetu wa leo ni Tanzania ya Afcon tukaribie hiki kitamu chakula tulichokingoja miaka kenda na kenda ! Na unakumbuka Tanzania iliyofuzu Afcon kwa mara ya kwanza ? ,ambapo Katika mechi hiyo, Taifa Stars iliwakilishwa na kipa Juma Pondamali,mabeki ni Leopard Tasso, Mohammed Kajole/ Ahmed Amasha, Salim Amir, Jella Mtagwa, viungo ni Leodegar Tenga, Hussein Ngulungu na washambulaji ni Omari Hussein, Peter Tino, Mohamed Salim na Thuweni Ally.


Kikosi hicho kilichokuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Joel Bendera na Ray Gama, ndicho kilichoiwakilisha Tanzania katika fainali za kombe hilo sasa 2019 umekuwa mwaka wa baraka nchini hasa upande wa soka tumeshuhudia Simba na Taifa stars zikifanya maajabu na labda tuwashukuru jirani Uganda na wangekua Ghana labda wangetuvalia miwani ya Mbao

wachezaji hawa wameingia kwenye historia Waliozama kambani Uwanja wa Taifa Simon Msuva dakika ya 21, Erasto Nyoni dakika ya 51 na Agrey Morris dakika ya 57 bil a kusahau wengine katika kikosi waliowakilishwa na Mbwana Samata popa au Samagoal ndoto zangu hawa wachezaji wawe nyoka wakali kwa vizazi vingine kama tulivyoona kwa wenzetu.

Sasa Tuweke kando uwenda wazimu na tuichukulie michuano hii ya Afcon tuliyopata karata kama mwanzo mpya wa mafanikio yetu katika kabumbu viongozi wetu wamekua watu wa lawama mno na visingizio kuliko mtendo emu tizama zama hizi za Kidigitali ligi yetu inakosa mdhamini lakini bado hakun sababu za msingi naona tukifanya vibaya Afcon utasikia ooh’ tumejithidi sio kweli ukishafuzu tu wewe ni mshindani sitaki kuamini na kusikia viongozi wakipigania tiketi za kwenda Misri Afcon kuliko kupigania maandalizi najua tuna kiu lakini tuzishike kiu zetu.

Hizi hapa faida za nchi kufuzu Afcon kwanza wachezaji pili nchi Tatu ,Biashara kwanza milango ya mawakala kwa wachezaji inakua mno kulingana na heshima ya michuano ,kwa nchi heshima inakua maradufu fursa ngingi na vipaumbele kutokea fifa zunakuja mfano miradi mbalimbali ya kukuza soka la vijana Grassroot, Na hadhaan inafahamika hapa na duniani soka umekua mchezo wa biashara dunia ya sasa na hapo watalii watamwagika tele emu tuache kuifanya Afcon iwe kichaka na tuitumie iwe nyoka

Na mwisho Tanzani imepangwa kundi c ikiwa na jirani zetu Kenya, Pia Algeria Vigogo hawa wa Kaskazini na Senegal nasemaje kila kitu tunacho vipaji na hamasa ndio silaha yetu lakini maandalizi ya timu ndio mzizi wa fitna twendeni Misri tukawe nyoka uzalendo Kwanza.

(Visited 39 times, 1 visits today)
Share this post