ASSAs

KUKATIKA KWA UMEME OVYO IMESABABISHA RAIS WA ZIMBABWE KUMUACHISHA KAZI WAZIRI WA NISHATI

261
0
Share:

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemfukuza kazi waziri wa nishati, Joram Gumbo kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara tangu mwaka 2016 ambapo nafasi ya waziri huyo amepewa naibu waziri wa usafirishaji na miundo mbinu Forune Chasi.

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali amesema siku ya jumatatu kuwa umeme ambao umekuwa ukikatika kwa saa tano au nane ni kutokana na upungufu wa maji katika mtambo mkubwa wa uzalishaji umeme, vilevile machimbo ya migodi yatahathirika na kukatika huko kwa umeme.

Mamlaka inalaumu kuzimika au kukatika kwa umeme huo kutokana na mtambo wa uzalishaji umeme kuzalisha umeme kwa kiwango kidogo kutokana na ukame ambao umesababisha maji kupatikana kwa kiwango kidogo.

Aidha serikali ya Zimbabwe imepanga kuagiza nishati kutoka nchi jirani ya Msumbiji na Afrika kusini.

Zimbabwe imekuwa ikipata tatizo la ukataji umeme tangu mwaka 2016
Siku ya jumatatu , kampuni ya uzalishaji umeme inayomilikiwa na serikali ilitangaza kuwa umeme utakatika kwa saa tano mpaka nane.

(Visited 14 times, 1 visits today)
Share this post