ASSAs

TAHARUKI YAZUKA TWARU, UKWELI WOTE HUU HAPA

398
0
Share:

Dar es Salaam

Chama Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kimekanusha taarifa iliyotolewa na Gazeti la Jahmuri toleo namba 398 la tarehe 14/5 mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Wamdanganya Magufuli’.

Akitoa ufanunuzi huo jijini Dar es salaam mapema leo hii, Mwenyekiti wa TWARU Lomitu – Ole Saitabau amesema taarifa iliyotolewa katika gazeti hilo ni ya uongo kwani kila kitu kilifanywa kwa kufuata sheria ila changamoto ilikua ni baadhi ya wafanyakazi kutoshikwa mkono na Rais John Magufuli.

Amesema kuwa, kilicholeta utata siku ya wafanyakazi duniani ambapo kitaifa yalifanyika Mbeya ambapo Rais John Magufuli alikua mgeni rasmi, sambamba na kuwashika mkono wafanyakazi bora waliochaguliwa na wafanyakazi wenzao, hivyo kutokana na muda mchache Rais Magufuli alilazimika kuwashika wachache.

Hata hivyo,amesema Chama chao kilipeleka majina matatu ya wafanyakazi Bora akiwemo Focas Sahani,Richard Hegani na James Kunena ambao walichaguliwa na Wafanyakazi .

“Wote walistahili kusomwa pale ispokua taarifa zilizotakiwa Ni kila chama kipepeke majina mawili kwani kulikua na majina 40 waliostahili kupewa zawadi zao na Rais John Magufuli lakini kutokana na muda walipatikana 26 kuwawakilisha wenzao”amesema Saitabau

Ameongeza kuwa, wanashangaa sana kuona taarifa ambayo haikua sahihi kwani wafanyakazi bora wote walipewa staiki zao na mwajiri wao na suala la chama kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyotolewa na gazeti hilo.

“Kwa wale wote hawakupata vyeti siku ile,vipo na vitatokewa na TUCTA I kupitia vyama vyao na watafanyiwa utaratibu wa kupatiwa malipo “amesema Saitabau

Aidha, amesema chama hicho kinaamini kua Rais John Magufuli ni wa watu wote habagui ndio maana hata wafanyakazi wanaoendana na kasi ya awamu ya tano wanachaguliwa kua wafanyakazi bora.

(Visited 18 times, 1 visits today)
Share this post