ASSAs

WAZIRI JANUARI MAKAMBA ATOA RAI KWA WAKUU WA MIKOA

299
0
Share:

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, mhe. Januari Makamba ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na mamlaka zingine zitakazo husika katika zoezi la kutokomeza biashara na matumizi ya bidhaa za Plastiki zilizopigwa marufuku.

Akizungumzia marufuku hiyo Makamba amesema kuwa katika awamu ya kwanza marufuku hiyo inahusisha mifuko ya plastiki tu huku bidhaa zingine zinazotumia plastiki vifungashio vya plastiki kuendelea kutumika wakati utaratibu ukiendelea. Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni bidhaa za chakula, kilimo na dawa.

Makamba amesema kuwa upo uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala ambapo kiwanda cha karatasi cha Mufindi kimesema åitaongeza uzalishaji zaidi ya mara tatu;

“ Tunao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala, wazalishaji wa mifuko hiyo wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi kimesema kitaongeza uzalishaji zaidi ya maratatu huku wawekezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine za kuzalishia mifuko hiyo,”Alisema Waziri Makamba.

Aidha Makamba amesema kuwa nchi ya Tanzania inaweza kufanikiwa katika zoezi hili kwa kuwa inazalisha mifuko mbadala ya karatasi ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa na nchi jirani za  Rwanda huku kenya wakitumia asilimia kubwa ya mifuko kutoka Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi cha hapa nchini, Kenya ikitumia asilimia 50, jambo linalotoa tafsiri kuwa tunaouwezo wa kuzalisha mifuko mbadala  itakayotosheleza,” Alisema Januari Makamba.

(Visited 23 times, 1 visits today)
Share this post