ASSAs

WAZIRI MKUU WA UINGEEREZA ATANGAZA KUJIUZULU

476
0
Share:

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May,  ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kuanzia leo, Ijumaa, Mei 24, 2019, kutokana na shinikizo la chama chake cha Conservative. May pia ametangaza kuwa atajiuzulu kukiongoza chama chake ifikapo Juni 7, 2019.

Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya “kila awezalo” kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Ni jambo linalosalia kuwa “na majuto mengi” kwamba ameshindwa kutimiza Brexit – Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.

Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.

Sauti yake ilittereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: “Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maihsani mwangu kuhudumu.

“Waziri mkuu mwanamke wa pili, na bila shaka sio wa mwisho.

“Nachukua hatua hii bila ya uovu wowote, bali na shukrani za dhati na kubwa kutokana na kupata fursa kuitumikia nchi ninayoipenda.”

(Visited 24 times, 1 visits today)
Share this post