ASSAs

MSHAMBULIAJI WA TANZANIA APATA DILI KUBWA KATIKA KLABU YA BLACKPOOL

1537
0
Share:

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf amesajiliwa na klabu ya Blackpool  ya nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo mwenye umri wa 27, anajiunga na timu hiyo inayoshiriki League One nchini England, akitokea Solihull Moors ambayo inayoshiriki National League ya nchini humo.

Adi ambaye amewahi kuitwa timu ya taifa ya Tanzania, amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo katika majira haya ya kiangazi.

(Visited 612 times, 1 visits today)
Share this post