ASSAs

TUHUMA ZA RUSHWA ZAMUWEKA MATATANI NYARANDU

1248
0
Share:

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) na Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kabla ya kuhamia Chadema, amekamatwa na kuchukuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wamekataa kujitambulisha akiwa kwenye kikao cha ndani cha CHADEMA kwenye Kata ya Itaja, wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida.

Nyalandu alikua kwenye zoezi la ‘Chadema ni msingi’ ambapo watu hao walifika wakiwa na silaha na kumchukua kwa nguvu na kutokomea nae kusikojulikana.

Wengine waliokamatwa ni Mwenyekiti wa kata hiyo na aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema wa jimbo hilo, David Jumbe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amesema taarifa hizo ni za uzushi; “Ndugu mwandishi umefanya vyema kuniuliza, watu wanazusha uongo mitandaoni, watafuteni TAKUKURU watawapa ukweli wa jambo hilo, polisi hawajamkamata.”

(Visited 86 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us