ASSAs

MCHUNGAJI AWAVAA MAASKOFU AWATAKA WAMUHESHIMU MKEWE

1184
0
Share:

Mchungaji maarufu nchini Kenya Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelist Ministry amegonga vichwa vya habari kwa mara nyengine tena baada ya kutishia kufunga matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism akidai kwamba maaskofu hawamuheshimu mke wake. 

Katika kanda ya video iliosambaa katika vyombo vya habari , anaonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafurusha wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda. 

”Wakati huu nitawaonyesha uwezo wangu… mwanamke yeyote ambaye hatamuheshimu mke wangu ….mulinipata hapa na wake zenu, mumejitajirisha kupitia juhudi zangu” . 

”Wajinga nyie…wajeuri…nilikuwa nikihubiri katika mkokoteni , naapa mbele ya Mungu nitawaonyesha Ng’ang’a ni nani….”. 

Mchungaji huyo anaonekana akiwaambia kwamba ni kinyume kwa wao kujigamba kuhusu utajiri waliojipatia kutoka katika kanisa lake na bado hawamuheshimu. 

”Nataka kuwaambia nyinyi maaskofu, iwapo hamutamuheshimu mke wanngu nitawafurusha katika kanisa langu. sitaki kujua wewe ni nani”, alisema mchungaji huyo. 

Ng’nga anasema kuwa amefikisha umri ambao anahitaji kuheshimika na maaskofu wote. Ninapo kohoa lazima mutii, alisema. Mchungaji huyo alisema kuwa anakabiliwa na changamoto kwa sababu shetani anataka kuliangusha kanisa lake. 

”Shetani anakabiliana nami kwa sababu anataka kuniangusha, hakuna kitu munachoweza kuniambia….Mimi ni Neno na ndio maana ninapigwa…. Sitawaruhusu nyinyi na wake zenu kunipatia msongo wa mawazo zaidi”,alisema. 

”Iwapo munataka kujiita maaskofu, munahitaji kufikiria kule mulikotoka, ni vipi munajigamba mbele yangu na mulikuja kwangu na umaskini…nitawafukuza nyie nyote… takataka’

(Visited 126 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us