ASSAs

MIKOA MINNE KUPULIZWA DAWA YA KUUA MBU

1433
0
Share:

Jiji la Dar na viunga vyake litaanza kupuliziwa dawa ya kuua wadudu (Biolarvicides) ikiwemo mbu pevu, ikiwa ni sehemu ya kupambana na ugonjwa wa homa ya dengue ambao hivi sasa ni tishio kwa wakazi wa Dar es Salaam. 

Zoezi hili pia litafanyika katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga ambayo pia imeripotiwa kukumbwa na athari za ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo Juni 2, 2019 wakati wa ziara maalum katika eneo la Jangwani jijini hapa iliyowakutanisha viongozi wa juu wa Waziri wa Afya wakiongozwa na Waziri, Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.

 Akizungumza baada ya ziara hiyo, Waziri Mwalimu ametoa maagizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) Aboubakar Kunenge kuhakikisha umwagiliaji dawa ya kuua wadudu ikiwemo mbu pevu unaanza mara moja. 

“Mvua zimeshamalizika sasa naagiza RAS muanze kupulizia dawa na zoezi hili halitazidi siku tano, mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga. Pia naagiza wamiliki wa baa, mahoteli, makanisa, misikiti na nyumba moja moja kuchukua hatua ya upuliziaji wa dawa hii,” amesema Mwalimu. 

Naibu Waziri wa afya Dk Faustine Ndugulile amezungumzia suala la mkanganyiko uliopo katika vipimo vya ugunduzi wa homa hiyo (dengue) na kusema hivi sasa vipimo hivyo ni bure katika hospitali zote za umma. Pia ametoa onyo kwa wamiliki wa hospitali binafsi ambao wamekuwa wakitoa majibu tofauti kwa wagonjwa kuhusu kipimo cha homa hiyo. 

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam  Abubakari Kunenge amesema tayari wameanza maandalizi muda mrefu na kilichokuwa kikisubiriwa ilikuwa ni mashine za upuliziaji wa dawa hiyo.

(Visited 171 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us