ASSAs

MWENYEKITI UMOJA WA VIJANA CCM LINDI AWAKUMBUKA WAHITAJI KATIKA SIKUKUU YA EID EL FITRI

1321
0
Share:

Mwenyekiti wa umoja Wa vijana ccm Mkoa wa Lindi comred Majid Lupanda, Leo tarehe 5/6/2019 ikiwa ni Siku ya Eid el- fitri amewatembelea na kutoa misaada kwa watu wenye maitaji maalumu

Mwenyekiti huyo alitembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Wilaya ya Nachingwea (WODA) nakutoa mchele kwa ajili ya sikukuu ya Eid,
Pia mwenye kiti alitembelea nyumba tofauti tofauti katika harakati za kutoa msaada wa chakula kwa wale wanye mahitajio hususani watu wenye ulemavu na pia kutokana na wengi wao kuwa katika maeneo mbalimbali Mwenyekiti aliamua kuweka kambi eneo la sokoni ambako watu wenye uhitaji maalumu huwa wanapita katika harakati za kutafuta ridhiki ili aweze kuwapata kitahisi, ambapo aliendelea kutoa msaada ili kuwafanya nao wafurahie siku hii adhim ya EID EL-FITR

Mwenyekiti ameyafanya hivyo kwa kutambua chama cha Mapinduzi kina amini binadamu wote ni sawa na Afrika ji moja, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwa karibu na kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji maalumu.

” Ikiwa Leo ni Siku ya eid hivyo kuna kila sababu ya watu wenye uwezo japo kidogo kuwajali na kuwasaidia watu wenye maitaji maalumu ili na wao waweze kufurahia sikukuu kama wanavyofurahi watu wengine waliojaaliwa kipato”

Mwenyekiti amewaomba watanzania wote kuwajali watu wenye mahitaji maalumu na kutambua kwamba sote ni ndugu moja.

Mwisho mwenyekiti amewatakia Eid Mubarak watanzania wote na kuomba tusherekee kwa Upendo na Amani
” MUNGU UBARIKI TANZANIA:

(Visited 120 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us