ASSAs

RIHANNA ATAJWA KUWA MWANAMUZIKI MILLIONEA WA KIKE DUNIANI

1924
0
Share:

Mwanamuziki kutoka Marekani  Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna amekuwa mwanamuziki wa kike tajiri zaidi Duniani kwa mujibu wa toleo jipya la jarida la Forbes.

Orodha hiyo mpya ya Forbes imeutaja utajiri wa Rihanna kufikia dola millioni 600 ambazo ni sawa na Trilioni 1.3 akifatiwa na Madonna mwenye utajiri wa  dola 570, Celine Dion akiwa na utajiri wa dola 450 huku Beyonce akiwa na kiasi cha dola 400.

Hata hivyo imetajwa kuwa utajiri mkubwa wa Riri ni nje ya mapato ya muziki na matamasha, utajiri huo umetokana na uwekezaji wake kwenye mitindo ikiwa ni pamoja na ushirikianio na kampuni ya kifaransa  ya LVMH na mapato yanayotokana na kampuni ya urembo ya Fenty Beauty.

Ukiachana na collabo zake za hivi karibuni ikumbukwe kuwa Riri anamwaka wa tatu sasa hajatoa wimbo wowote tangu alipoiachia albamu yake ya ANTI mwaka 2016.

(Visited 259 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us