ASSAs

WALIOTEULIWA KUAPISHWA LEO IKULU

1667
0
Share:

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kesho Juni 10, 2019 atawaapisha viongozi wateule wawili ambao ni, Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Charles Kicheere.


Tukio hilo litafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8:00 mchana, ambapo pia atashuhudia tukio la makabidhiano ya fedha kutoka Airtel kwenda serikalini kiasi cha shilingi bilioni 5.27.

Miongoni mwa fedha zitakazotolewa, shilingi bilioni 2.27 ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo wakati Shilingi bilioni 3 ni malipo ya kila mwezi yatokanayo na umiliki wa hisa za Airtel Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel International.

Mapema asubuhi ya Juni 8, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Joseph George Kakunda, na kumteua Mh. Innocent Lugha Bashungwa kushika nafasi hiyo.

(Visited 185 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us