ASSAs

MSAMA ATOA OMBI KWA WAFANYABIASHARA KOTE NCHINI

1528
0
Share:

Mkurugenzi wa msama promotion Alex Msama amewahimiza wafanyabiashara nchini kulipa kodi kwa hiara ili kuweza kukuza uchumi pamoja na kuimarisha miundombinu ya nchi.

Msama amezungumza hayo alipokuwa akizungumza na waandsihi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema wafanya biashara kulipa kodi pia ni njia moja wapo ya kumuunga mkono Rais.

“naomba wafanyabiashara wenzangu kote nchini tulipe kodi kwa hiyari ili kumuunga mkono Rais wetu Magufuli katika kujenga nchi yetu kila mtu anaona jinsi Serikali inavyohudumia wananchi wake kwenye elimu, Afya hata kwenye miundombinu tunaona barabara zikijengwa.

wafanyabiashara wenzangu tusiwaone watu wa TRA kama maadui zetu Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa mahusiano mazuri kati yetu na TRA hivyo tuwe wazalendo kwa kulipa kodi bila kusubiri kulazimishwa na maofisa wa TRA kwani kodi ndiyo inajenga nchi”amesema.

Pia ametoa ushari kwa Waziri mpya wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, kutembelea wamiliki wa viwanda ili kufanya mazungumzo nao ili kuweza kufahamu changamoto zao na kuzitatua.

“Ushauri wangu kwa Waziri mpya wa Viwanda na biashara namshauli awatembelee wamiliki wa viwanda na kuzungumza nao ajue changamoto zao na jinsi ya kuzitatua pia awape ushirikiano watu wanaotaka kuanzisha viwanda awe tayari kupokea malalamiko na ushauri muda wote”

June 10,2019 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisisitiza makampuni na wafanyabiashara kulipa kodi bila kukwepa ili kuweza kleta maendeleo ya nchi.

(Visited 170 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us