ASSAs

BREAKING: NDAYIRAGIJE KOCHA MKUU MPYA AZAM FC

813
0
Share:

Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo umeingia mkataba wa miaka miwili na kocha Etienne Ndayiragije, kwa ajili ya kuinoa timu hiyo kuanzia msimu ujao.

Ndayiragije anachukua nafasi ya makocha wazawa, Abdul Mingange na Idd Nassor Cheche, waliokuwa makocha wa muda wa timu hiyo hadi kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kusitishiwa mkataba kwa Hans Van Der Pluijm na Juma Mwambusi.

Zoezi la kocha huyo kuingia mkataba limefanyika ofisi za Mzizima, mbele ya waandishi wa habari, Azam FC ikiwakilishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Mratibu Phillip Alando.

Kocha huyo anatarajia kuanza kukinoa kikosi hicho kuanzia Juni 20 mwaka huu, Azam FC itakapoanza maandalizi ya msimu mpya na kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame ikiwa kama bingwa mtetezi.

(Visited 64 times, 1 visits today)
Share this post