ASSAs

KAKA WA KIM JONG-UN ALIYEUAWA, ALIKUWA JASUSI WA CIA

1519
0
Share:

Imeripotiwa kwamba kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un,  aliyeitwa Kim Jong-nam aliuawa kwa sumu akiwa safarini nchini Malaysia mwaka 2017, baada ya kubainika kuwa ni jasusi wa shirika  la ujasusi la Marekani CIA.

Gazeti la Wall Street Journal, limechapisha ripoti hiyo Jumatatu na kusema limedokezwa hayo na mtu mwenye taarifa kamili kuhusu tukio hilo na kwamba kulikuwa na mawasiliano baina ya CIA na Kim Jong-nam.

Uchunguzi uliofanywa na Malaysia kuhusu kesi hiyo mwaka jana uligundua kuwa, Kim Jong-nam alikutana na raia mmoja wa Marekani, aliyeshukiwa kuwa ni jasusi, katika hoteli moja nchini Malaysia siku nne kabla ya kuuawa tarehe 9 Februari 2019.

Kabla ya hapo, raia mmoja wa Indonesia, Siti Aisyah, na raia mmoja wa Vietnam, Doan Thi Huong, walikuwa wamekamatwa kwa tuhuma za kumpa sumu Kim Jong-nam katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, lakini waliachiliwa huru mapema mwaka huu nchini Malaysia baada ya kukosekana ushahidi.

(Visited 225 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us