ASSAs

UMEME KUWASHWA MUDA SIO MREFU NDANI YA KATA ZA KIEGEI NA MATEKWE.

954
0
Share:

Katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma muhimu za kijamii katika vijiji vyetu vya wilaya ya Nachingwea, kampuni ya POWERCORNER ikishirikiana kwa karibu na Serikali inakwenda kukamilisha mradi wa umeme wa jua muda sio mrefu na hivyo kwenda kuwapa huduma wananchi wa maeneo hayo ambayo wako mbali na makao makuu ya mji na hivyo kuweka historia iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu .

Nawashukuru sana kampuni ya POWERCORNER kwa kuitikia wito na maombi yetu ya kutuletea huduma hii muhimu ktk kuharakisha shughuli za maendeleo Natambua changamoto nyingi mlizopitia hadi kufikia hatua hii muhimu .

Aidha huduma kama hii ya kuwasha na kusambaza umeme kupitia REA AWAMU YA TATU inaendelea katika vijiji vya mnero Ngongo,Mnero Miembeni,Mchangani,Ndomondo,Nampemba,Mkukwe,Nango’ndo ,Mpiruka ,lionja,Ngunichile,Chingunduli,Mkatapory Kihuwe nk

Awamu ya tatu B itafanyika katika vijiji vingine vilivyobakia kupata huduma hiyo muhimu .

Tulihaidi tunatekeleza

Nachingwea ni yetu sote

Mwl Masala
Dodoma
Tanzania
12/6/2019

(Visited 61 times, 1 visits today)
Share this post