ASSAs

BILLIONI 880 KULIPWA KWA WASTAAFU

274
0
Share:

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umefanya malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 880 kwa wastaafu elfu 10,000 ambao walikuwa wanadai malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi.

Hayo yamebainishwa na Meneja Kiongozi wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ambapo amesema malipo hayo yamefanyika katika kipindi cha mpito kilichotolewa na Serikali kuanzia  Agosti 2018 hadi Februari 2019.

amesema kuwa hatua hiyo ni mwaka mmoja, tangu mfuko huo uanze kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 baada ya Serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

“Ili kuhakikisha PSSSF inatoa huduma bora na za haraka, imefungua ofisi mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na tunatoa wito sasa, kwa wale wastaafu takriban elfu 10,500 ambao bado taarifa zao hazijahakikiwa wafike kwenye ofisi zilizo karibu nao ili kukamilisha zoezi hilo muhimu linalofanyika kila mwaka.”

Kuhusiana na suala la uhakiki, kiongozi amesema kuwa “Lengo la uhakiki ni kuupa Mfuko fursa ya kufanya malipo kwa usahihi na kwa mtu anayepaswa kulipwa kwani taarifa zinaweza kubadilika ikiwa ni pamoja na zile za kibenki huenda mhusika akahama kutoka benki moja kwenda nyingine, mabadiliko ya wategemezi lakini hata kifo pia.”

Play this Game for 1 Minute and see why everyone is addictedDesert Order|SponsoredNew WiFi Booster Takes Dar-es-salaam By StormMoney News Tips|SponsoredWant to Speak Spanish, French or even Arabian? We have a simple solution for …MUAMA Instant Translator|SponsoredLanguage Translator Device Takes Tanzania, United Republic Of By StormTranslaty Pro|Sponsored

New Website Finds the Cheapest Flights from Dar Es SalaamTrips Shop|SponsoredThe Most Beautiful Royal WomenHooch|SponsoredRichest Pastors in Africa 2018 – Check Out Who Is From Tanzania, United Republic OfEverydaychimp|SponsoredFahamu viongozi walioteuliwa na Rais Magufuli | East Africa TelevisionEATVMarais 19 kuwasili Tanzania | East Africa TelevisionEATV

TOP STORIES

Sport“Shughuli ya Lechantre imekwisha”-Manara

SportNgoma ashindwa kuichezea Azam, Kagame

Current AffairsAmuua mke mwenza na kumzika shambani

Current AffairsMbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM

MOST POPULAR

Current Affairs Viongozi wa umma Arusha, DSM kuchunguzwa

Current Affairs Mahakama yaamuru Wema Sepetu akamatwe

Current Affairs Mbunge CCM amtofautisha Lissu na Nyalandu

Current Affairs Bashe amchambua mteule wa JPM

Current Affairs Serikali yapandisha ushuru wa nywele za bandia

ABOUT US

Network

© 2019 East Africa Television Limited. All Rights Reserved

(Visited 18 times, 1 visits today)
Share this post