ASSAs

CHAMA CHA MAPINDUZI CHATOA OFISI KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) MOROGORO.

269
0
Share:

Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akitoa Salam za Chama Cha Mapinduzi katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) Alkhamis 13 June 2019

Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe.

“Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi ni binadamu kama binadamu wengine wanaostahili kupewa heshima zote wakiwa binadamu na watu huru” Shaka

“Kitendo chochote cha kuwabagua watu wenye ulemavu wowote ukiwemo wa ngozi ni zaidi ya ubaguzi. Ni makosa, haramu na kumkosea mungu wetu” Shaka

“Tulipokea kilio cha wenzetu wenye ulemavu wa Ngozi mkoa huu hawana sehemu ya kufanyia shuhuli zao hivyo Chama Cha Mapinduzi kinatoa majengo ya ofisi kuwapatia ili muweze kuendesha shuhuli zenu, sisi ndio wenye ilani na kwenye ilani tumeainisha namna tutakavyounga mkono jitahada za watu wenye ulemavu katika kujiletea maendeleo, njoo tuwakabidhi ofisi mchape kazi kuunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli” Shaka

(Visited 16 times, 1 visits today)
Share this post