ASSAs

MAKAMBA AFUNGUKA SABABU ZITAKAZOMFANYA KUWA RAIS

770
0
Share:

Waziri wa Muungano wa Mazingira January Makamba amesema suala la yeye kuwa Rais wa Tanzania halitegemei mtu bali ni uwezo Mungu, endapo atakuwa amempangia kushika nafasi hiyo ya juu ya nchi.

Waziri Makamba ameandika hayo kupitia ukurasa wake twitter wakati akimjibu moja ya wafuasi wake ambapo alimueleza kuwa endapo akishindwa kuwa Rais wa Tanzania itakuwa amefanyiwa hujuma.

Akijibu swali hilo Waziri Makamba amesema kuwa “kuhusu kuwa Rais hili linasemwa sana nami niseme, kwangu na kwa wasionikubali hili jambo sio la kupania kwani Mungu ndiye hupanga, akitaka uwe hakuna awezaye kuzuia usiwe, na hadi mbingu na ardhi zitakula njama ili uwe, asipotaka uwe, hata ufanyeje huwezi”

Hivi karibuni Waziri Makamba alitangaza kupiga marufuku zoezi la utumiaji wa mifuko ya plastiki, kufuatia kuanza kutumika kwa kanuni mpya za zinazopiga marufuku utumiaji wa mifuko hiyo.

(Visited 88 times, 1 visits today)
Share this post