ASSAs

HILI NDILO ONYO KWA WATU WANAOTUMIA MIFUKO YA MIKATE

587
0
Share:

Baraza la Uhifadhi wa Mazingira nchini NEMC limesema halitamvumilia mtu ambaye atabainika kutumia mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na Serikali na kueleza kuwa atakayebainika atahukumiwa kwa mujibu wa sheria inavyosema.

Kauli hiyo imetolewa na Wakili wa NEMC, Vincent Haule ambapo aliulizwa swali kuhusiana na vifungashio vya mikate kutumika kama vifungashio vya bidhaa nyingine ambapo amesema atakaefanya hivyo atapewa adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria;

“mtu atakayejaribu kufanya hivyo anahitaji adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria, atakuwa amefanya kosa kwa makusudi, atatozwa faini ya laki 2.”

Suala la kutumia mifuko ya plastiki lilikatazwa kutokana na kuharibu mazingira kwakuwa mifuko hiyo haiozi ardhini.

(Visited 51 times, 1 visits today)
Share this post