ASSAs

RAIS WA ZAMANI WA MISRI MOHAMED MORSI AZIKWA

703
0
Share:

Na Leandra Gabriel, Blogu ya JamiiHATIMA ya aliyekuwa Rais wa Misri Mohamed Morsi (68) imehitimishwa kwa kuzikwa leo huko Mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Cairo kijana wake amethibitisha.
Morsi amezikwa na ndugu zake wa karibu baada ya kukutwa na umauti kwa kuanguka ghafla akiwa mahakamani.

 Kituo cha habari Aljazeera kimeeleza kuwa Morsi amezikwa leo asubuhi na waumini wa Muslim Brotherhood pamoja na ndugu wa karibu na kupitia ukurasa wake wa Facebook kijana wa marehemu Ahmed Morsi amethibitisha.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na ndugu na waumini hao wa Brotherhood Muslim huko Mashariki mwa mji huo kwa kile kilichoelezwa kuwa mamlaka nchini humo kuzuia mazishi hayo yasifanyike nyumbani kwa Morsi huko Sharqiya.

“Tuliosha mwili wake katika hospitali ya gereza la Tora, tukamswalia katika msikiti wa magereza na amezikwa katika misingi ya kiislamu” ameandika Ahmed.
Wakili wa Morsi Abdel Moneim amethibitisha kuwa mazishi yamefanyika Al- wafaa wa al- Amal.
Morsi alikuwa Rais wa kwanza kuchanguliwa kidemokrasia nchini humo mwaka 2012 baada ya  kuondolewa kwa Hosni Mubarak aliyetawala kwa miaka 30.
Hata hivyo hakudumu madarakani kwani aliondolewa kwa jeshi na maandamano yakiongozwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo Abdel Fattah el- Sisi mwaka 2013 na baadaye kushikiliwa hadi umauti ulipomkuta.

(Visited 116 times, 1 visits today)
Share this post