ASSAs

JINA LA JAMES KOTEI LATUA YANGA

997
0
Share:

SIMBA na Yanga zote zipo kwenye mikakati mipya ya kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao, kila upande unaonekana kuwa na maandalizi makubwa kwa kuwa wote watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati maandalizi hayo yakiendelea, habari za ndani ya klabu zinadai kuwa kiungo mkabaji wa Simba Mghana, James Kotei hana nafasi ya kuendelea kuichezea timu hiyo, hali ambayo imesababisha jina lake lianze kutajwa ndani ya Klabu ya Yanga kwa nia ya kumsajili.

Mghana huyo ni kati ya wachezaji waliomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu uliopita na inaelezwa kuwa uongozi wa Simba umepanga kuachana na kiungo huyo mkabaji anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi. Wachezaji wengine wanaotajwa kuachwa na Simba ni Muivory Coast, Zana Coulibaly, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mganda Juuko Murshid na Waghana, Asante Kwasi na Nicholas Gyan.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, uongozi wa Yanga upo kwenye majadiliano kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba.

(Visited 97 times, 1 visits today)
Share this post