ASSAs

RC MAKONDA; KENYA LAZIMA WAPIGWE

482
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametamba kwamba Kenya lazima wapigwe ambapo aliyasema hayo wakati alipotembelea jana kambi ya Stars wakati ikiwa inajiandaa na mechi hiyo na Kenya. 

Akizungumza wakati yupo kambini hapo, Makonda amesema amewakuta wachezaji wa Stars wana ari ya juu na wameahidi ushindi mbele ya Kenya. “Wakenya kesho (leo) lazima wakae, nimekutana na wachezaji na wapo kwenye ari ya juu sana. 

“Kipigo ambacho tuliwapa Uganda ndiyo hicho ambacho tutawapa, kwenye michuano hii sisi tumekuja kufanya kazi, tutashinda mechi hii na nyingine zinazofuata na ikiwezekana tutatwaa ubingwa,” alisema Makonda.

Stars inayofundishwa na kocha Emmanuel Amunike leo Alhamisi itacheza mechi yake ya pili ya Afcon baada ya ile ya kwanza kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal. 

(Visited 33 times, 1 visits today)
Share this post