ASSAs

BAADA YA KUFUNGWA KWA TAIFA STARS, SAMATTA AFUNGUKA HAYA.

2516
0
Share:


Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amesema moja ya makosa ambayo yalipelekea timu ya taifa ya Tanzania kupoteza mchezo wake wa dhidi ya Kenya, ni wachezaji wa Tanzania kushindwa kulinda ushindi ambao waliupata kwenye kipindi cha kwanza. 

Nahodha Samatta amefunguka hayo nchini Misri ikiwa ni saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo ambao Stars ilifungwa kwa taabu bao 3 -2 na kusema kuwa timu nzima walishindwa kulinda ushindi wao na anammini kuanguka ni kujifunza.

“Mimi nafikiri ni timu nzima tulishindwa kulinda ushindi wetu, bado tupo kwenye mashindano naamini siku zote kuanguka ni kujifunza, sisi tupo na tunaendelea kupambana, kama Mungu yupo na sisi tunaendelea kumwamini, nadhani Watanzania tumewaangusha sana na tungeweza kuwa na matokeo chanya leo.” amesema Capt. Samatta

Katika mchezo jana mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Simon Msuva kunako dakika ya 6 huku bao la pili la Stars likifungwa na Mbwana Samatta akifunga dakika ya 40.

(Visited 1,083 times, 1 visits today)
Share this post