ASSAs

HIVI NDIVYO KIUNGO NIYONZIMA ALIVYOIAGA SIMBA

673
0
Share:

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amewaaga mashabiki wa timu hiyo na kuwashukuru kwa yote waliyoshirikiana kwa kipindi cha misimu miwili ndani ya klabu hiyo.

Mkataba wa Niyonzima wa miaka miwili na Simba umemalizika hivi karibuni .

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Niyonzima aliandika ujumbe mfupi wenye maneno ya kuwaaga mashabiki wa Simba, ujumbe wake ulisomeka hivi: “Nawashukuru kwa kumbukumbu tulizoweka pamoja, kadiri muda unavyokwenda ndiyo nitaweka wazi sehemu nitakayokwenda.”

Ikumbukwe Championi iliweka wazi mapema hatima ya mchezaji huyo ndani ya kikosi hicho kufuatia viongozi wa juu kunishikiza kutoongezewa mkataba mpya kutokana na madai ya kuwa msumbufu.

(Visited 128 times, 1 visits today)
Share this post