ASSAs

DC MJEMA APEWA TUZO NA WAMACHINGA ILALA

294
0
Share:

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amepewa tuzo na Wafanya biashara ndogondogo (wamachinga) wa Wilaya ya hiyo kwa lengo kutambua mchango wake kwa kuwaunganisha na kuwaweka katika utaratibu maalum wa kufanya kazi.

Akizungumza katika hafla fupi Wilayani Ilala leo,Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema alisema Wamachinga amewatoa katika daraja la chini sasa wapo katika daraja la kati sasa wafanye kazi ili walete maendeleo ya Taifa letu wafikie malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli Uchumi wa viwanda.

“Wamachinga wa Wilaya ya Ilala tumewaweka katika utaratibu unaotambulika wa kufanya biashara katika mitaa yao ni sehemu ya jukumu langu kama sehemu ya kazi na wote wanavitambulisho vya Wafanyabiashara “alisema Mjema.

Mjema aliwataka Wamachinga wa Wilaya ya Ilala kuanzisha viwanda vidogovigo kwa ajili ya shughuli za uzalisha ili wajikwamue kiuchumi.

Aliwataka wawe wafanyabiashara wakubwa watambulike Kimataifa wasiishie katika biashara ya Machinga.

“Natumia nafasi hii kuwashukuru wamachinga kwa
Kunipatia cheti maalum hiki kwa kutambua mchango wangu jinsi nilivyowatumikia katika wilaya hii”alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wamachinga Wilaya ya Ilala Steven Lusinde ,alisema uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 wamachinga watazunguka nchi nzima kumpigia kampeni Rais John Magufuili ili aongoze awamu ya pili.

“Tunakuomba Rais John Magufuli ifikapo mwaka 2020 wakati wa uchaguzi tunaomba nenda uchukue likizo sisi Wamachinga wa Wilaya ya Ilala tunakuakikishia ushindi mnono tutazunguka kwa ajili yako”alisema Lusinde.

Lusinde alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali kwa kuwatambua Wamachinga nchi nzima, na kuwawekea mazingira mazuri ya kazi sasa wanafanya shughuli zao kifua mbele bila usumbufu.

Aliwataka Watanzania kushirukiana na serikali ya awamu ya tano inatekeleza Ilani kwa vitendo kwa na usimamiaji miradi mikubwa ya kisasa.

(Visited 27 times, 1 visits today)
Share this post