ASSAs

UMOJA WA WAJANE VINGUNGUTI WAMPONGEZA KUMBILAMOTO

795
0
Share:

Dar es Salaam

Umoja wa wajane waishio Kata ya Vingunguti Manispaa ya Ilala wamempongeza Diwani wa kata hiyo Omary Kumbilamoto kwa kuwaletea walimu wa ujasiriamali kwa lengo la kuwawezesha kupata mafunzo ya kuweza kufanya biashara na kujiingizia kipato.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mapema leo hii wakati wakipatiwa mafunzo hayo, mmoja wa wajane hao, asenga Mohammed amesema kuwa Diwani huyo amekua akijitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanakua na maisha mazuri licha ya ukiwa walionao.

Amesema kuwa, wanamshukuru sana Diwani huyo kwani mafunzo hayo yataweza kuwaongezea ujuzi wa kufanya biashara hasa ukizingatia mali ghali nyingi za utengezaji wa bishara hizo yanapatikana nchini hususani katika mazingira yao wanayoishi

“Kupitia mafunzo haya tutaweza kuondokana kabisa na hali ya utegemezi, tutaweza kujitegemea wenyewe kwani tutakua tunazalisha biashara na kuziuza na kupata pesa, Diwani huyu ni mfano wa kuigwa katika jamii”amesema Asenga

Ameongeza kuwa”Leo tumepata mafunzo mbalimbali ikiwemo utengezaji wa mishumaa ya kuulia mbu, kutengeneza mafuta ya kujipaka pamoja na kutengeneza sabuni ya kufulia ambapo hii itatuingizia pesa kila siku”

(Visited 61 times, 1 visits today)
Share this post