ASSAs

‘MIMI SIO MTU WA KUMUONGELEA YOUNG DEE,SINA MUDA WA KUMUONGELEA MTU AMBAYE NIMESHAMKANYAGA’ AMBER LULU

453
0
Share:

Msanii wa Bongo Fleva, Amber Lulu amedai kuwa kwa sasa ‘level’ zake sio sawa na wapenzi wake wa zamani Young Dee na Prezzo.

”Mimi sio mtu wa kumuongelea Young Dee, sasa hivi mimi ni mtu wa kumuongelea Jay Z, Omarion, Chris Brown na Wiz Khalifa, sina muda wa kumuongelea mtu ambaye nishamkanyaga, hata hapa siwezi kumuongelea Prezzo ni babu kashazeeka sio ‘level’ zangu.”

Amber Lulu pia ameweka wazi ujio wa mtoto mpya baada ya kuonekana tumbo lake kuwa kubwa ambapo alisema, ”mimi ni mzuri, ukiniangalia juu mpaka chini, achana na kitambi huyu ni mtoto wenu mpya anakuja”.

Pia Amber Lulu amesema yeye ndio msanii wa kwanza wa kike kutoa milioni kumi kwenye video, hana shida na gari pesa hizo angekuwa msanii mwingine angenunua hata gari, bado anatembea kwa miguu na bajaji. 

(Visited 116 times, 1 visits today)
Share this post